LICHA ya kikosi cha Tottenham Hotspur kuanza kwa kupokea kichapo kwenye mchezo wake wa kwanza uwanja wa nyumbani wa Spurs wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Ajax, Meneja wa Spurs, Pochettino amesema bado wana nafasi ya kusonga mbele.
Pochettino amesema bado wana matumaini ya kutinga hatua ya fainali kwani kufungwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 15 na Donny Van de Beek kwao sio ajabu, wanajioanga mchezo wa marudio kupata matokeo.
"Matumaini yetu yanaishi, mchezo wetu wa marudio utakuwa mgumu ila upo wazi kwetu kushinda na kusonga mbele.
"Kwa sasa tunajiaadnaa na mchezo wetu wa pili, tutajaribu kushinda licha ya ugumu ambao utakuwepo kwetu ila sio sisi peke yetu hata wao pia utakuwa mgumu," amesema Pochettino.
Mchezo wa marudio utachezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Armsterdam arenA.
Historia inamkataa Spurs kufuzu hatua ya fainali kwani katika historia ya timu 17 ambazo ziliwahikufungwa nyumbani katika mchezo wa kwanza wa hatua y a nusu fainali hazikuweza kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa hata Ulaya.
0 Comments