Windows

Mo apongeza viongozi wapya Yanga, awapa changamoto



Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amewapongeza viongozi wapya wa Yanga waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika May 05 jijini Dar es salaam

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mo amewatakia kila la kheri viongozi hao huku akiwapa changamoto ya kuiboresha Yanga ili iwe mshindani wa kweli wa Simba katika kuwania mataji mbalimbali nchini

"Nawapongeza Yanga kwa changamoto chanya ya harakati za ubingwa kwa Simba pia nawapongeza viongozi wote wa Yanga waliochaguliwa na kuwatakia kila lakheri waifanye Yanga iwe imara ili iweze kuipa Simba changamoto kwa maendeleo ya soka letu," amesema


Uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla kwa kushirikiana na benchi la ufundi, tayari uko katika mchakato wa kuiboresha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao

Yanga inakusudia kutumia kati ya Bil 1.5 hadi Bil 2 kwa ajili ya usajili, kiasi cha fedha ambacho ni zaidi ya kile kilichotumika kuiboresha Simba msimu uliopita

Fedha hizo zitatokana na michango ya wadau wa Yanga ambao katika kipindi hiki cha mpito wameamua kuisimamia timu wao wenyewe kupitia kauli mbiu ya "TIMU YA WANANCHIWAWEKEZAJI NI WANANCHI"

Post a Comment

0 Comments