Baada ya kuibuliwa tetesi kuwa Yanga inawawania wachezaji watatu wa Simba Aishi Manula, Clatous Chama na Jonas Mkude katika mitandao ya kijamii wengi wameonekana kubeza tetesi hizo wakiamini Yanga haina uwezo wa kuwasajili wachezaji hao
Lakini wengi wasichofahamu usajili ni makubaliano baina ya mchezaji na timu husika. Mara nyingi makubaliano hayo huwa ni siri
Sio ajabu kwa mchezaji kuhusishwa na timu nyingine, kazi ya mchezaji ni kusakata kabumbu
Wengi wanaobeza hawajui Yanga imejipangaje kusajili msimu huu
Wengi wanaamini mfumo huu wa 'kutembeza bakuli' hauwezi kuipa Yanga uwezo wa kusajili mchezaji wamtakaye
Lakini wiki iliyopita uongozi wa Yanga uliahidi kumsajili mchezaji yeyote atakayependekezwa na kocha Mwinyi Zahera hata kama yuko nje ya nchicut
Inafahamika Simba iko katika wakati mgumu wa kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji wake kutokana na gharama za usajili wao kuwa juu
Simba ina idadi ya wachezaji karibu 15 ambao mikataba yao imemalizika na wengi wametumika katika kikosi cha kwanza
Wachezaji hao waliomaliza mikataba wametaka kuboreshewa maslahi katika mikataba mipya
Mkude, Manula na Chama ni miongoni mwa wachezaji waliogoma kusaini mikataba mipya wakitaka waongezwe fedha za usajili
Inaelezwa Yanga iko tayari kutoa ofa nono zaidi ya walizoahidiwa na Simba ili kuwasajili
Wakati Simba ikipambana kumn'goa Ajib Yanga, wafahamu Yanga pia haitakaa kimya
0 Comments