Windows

Kocha Ndanda ajivunia rekodi ya pekee



KOCHA Mkuu wa Ndanda FC, Khalid Adam, amejivunia rekodi aliyoweka katika kikosi hicho tangu alipokabidhiwa majukumu kipindi cha dirisha dogo la usajili msimu huu.

Rekodi aliyoweka kocha huyo ni kuitoa timu hiyo katika nafasi za mwisho na kuiwezesha kuwa miongoni mwa timu 10 bora hadi sasa, ikishika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tangu Ndanda imeanza kushiriki ligi hiyo huu ukiwa ni msimu wa tatu, imekuwa ikimaliza ligi huku ikiponea chupuchupu kushuka daraja.

Akizungumza na BINGWA jana, Adam, alisema anajivunia rekodi aliyoweka kwa kuwa akishinda mechi ya mwisho watamaliza ligi wakiwa nafasi ya sita, mafanikio ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wengine.

Alitaja siri ya mafanikio kuwa ni ushirikiano uliopo kati ya wachezaji, viongozi, mashabiki na benchi la ufundi tangu walipoanza mzunguko wa pili.

“Ninashukuru kwa hatua niliyofikia, ila niwashukuru klabu ya Ndanda kwa ushirikiano wao kuanzia ngazi ya juu hadi wachezaji kwani wamekuwa wakipambana katika kila mechi,” alisema Adam.

Kwa sasa Ndanda inashika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 37, ikishinda mara 12, sare 12 na kufungwa 13.

Ndanda ilianza kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2014/15 ambao ilimaliza nafasi ya tisa kati ya timu 16 ikiwa imevuna pointi 31.

Msimu wa 2015/16 ilimaliza ya tisa baada ya kuvuna pointi 35, msimu wa 2016/17 ilikuwa nafasi ya 13 ikiwa na alama 33, wakati msimu uliopita ilinusurika kushuka daraja kutokana na ushindi wa mechi ya

Post a Comment

0 Comments