

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere ameibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2018/19
Kagere ametwaa tuzo hiyo baada ya kufikisha mabao 23
Salim Aiyee wa Mwadui Fc ameibuka kwenye nafasi ya pili akiwa amefunga mabao 18 akifuatiwa na Heritier Makambo wa Yanga mwenye mabao 17
Wanafuata washambuliaji wawili wa Simba John Bocco mwenye mabao 16 na Emmanuel Okwi mwenye mabao 15
Kagere amesema haikuwa kazi rahisi kushinda tuzo hiyo.
Amewashukuru wachezaji wenzake katika kikosi cha Simba kwa ushirikiano waliompa na kiufanikiwa kuondoka na kiatu cha dhahabu
Kagere amewapongeza wenzake baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo



0 Comments