

Kwa mjibu wa takwimu kutoka Bodi ya Ligi kabla ya michezo ya leo, tofauti ya mabao ya Stand United ilikuwa -9 na ya Kagera Sugar ilikuwa -11
Baada ya matokeo ya leo ambapo JKT Tanzania imeifunga Stand United mabao 2-0 huku Mbao Fc ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar, timu hizo zinakuwa na tofauti sawa ya mabao -11
Matokeo ya michezo miwili timu hizo zilipokutana ndiyo yameamua ipi inapaswa kushuka daraja
Matokeo ya mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa mkoani Shinyanga, Stand United na Kagera Sugar zilitoka sare ya bao 1-1 wakati Stand United ilishinda kwa mabao 3-1 mchezo wa duru ya pili uliopigwa Kagera
Kwa mjibu wa takwimu hizo African Lyon na Kagera Sugar zimeshuka daraja moja kwa moja na Stand United na Mwadui FC zinacheza Play Off dhidi ya Pamba Fc na Geita Gold



0 Comments