![](https://4.bp.blogspot.com/-oWBF5rnYXzE/W7uedCj85EI/AAAAAAAAJdY/0jTfLk_9khU5DTaZ6o-KfH_A3hrpI_ZJQCLcBGAs/s320/aaaaaaaaaa.jpg)
![](https://1.bp.blogspot.com/-5UdUkBxLqPE/W7ujeNJL4XI/AAAAAAAAJds/dBugYDvLQq0WptS1YBXQGjJB_vJFBWL7wCLcBGAs/s320/yyyyyyyyyyyy.jpg)
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka wachezaji wa timu hiyo wajitume na kuwahakikishia timu nyingi ndani na nje ya Afrika zinaitupia jicho klabu hiyo kuangalia wachezaji wa kusajili
Dk Msolla ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu tangu aliyekuwa mshambuliaji wake Heritier Makambo kusajiliwa na Horoya AC ya Guinea
Aidha Dk Msolla amefichua kuwa sio Horoya AC pekee iliyokuwa inamuwania Makambo, kuna timu nyingine kutoka Ubelgiji inayotaka huduma ya mchezaji huyo
Yanga inatarajiwa kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mauzo ya mchezaji huyo ambapo Dk Msolla amesema wanawasubiri Horoya AC jijini Dar es salaam kumalizana nao
Inaelezwa Makambo amesaini mkataba wa awali wa miaka mitatu kukipiga na Horoya AC lakini kama timu kutoka Ubelgiji itatoa ofa nzuri zaidi huenda akauzwa huko
Dau la Horoya linadaiwa kuwa dola laki moja (zaidi ya Mil 230 za Kitanzania)
cut
"Nimewaambia wachezaji wangu kuwa hapa Yanga ni pazuri, ukionyesha juhudi tu unapata soko. Makambo amejituma na ndio maana sasa anatakiwa na klabu nyingi, ukiacha Horoya kuna klabu ya Ubelgiji imeleta barua, tutaona ni timu gani imeleta kubwa", DK Msolla amenukuliwa na Mwanaspoti
Mbali na Makambo, kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' naye ataondoka nchini wakati wowote kuelekea Uingereza kufanya majaribio katika moja ya timu inayoshiriki ligi daraja la pili
Uongozi mpya wa Yanga umeweka wazi kuwa hautasita kufanya biashara na timu zinazowania wachezaji wake (wenye mikataba) kama zitawasilisha ofa nzuri
Kwa habari zaidi Download App ya Mwana Jangwani kutoka Play Store. Bonyeza picha hapa chini
Habari hii Imesomwa mara 2993

0 Comments