

Aliyekuwa mlinda lango wa Yanga Beno Kakolanya amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya kutangazwa rasmi kuwa mchezaji huru kufuatia tukio lililopelekea kuvunjwa kwa mkataba wake
Kakolanya alikuwa na mgogoro na viongozi wa Yanga kufuatia mgomo aliofanya ambao ulipelekea kuenguliwa kikosini na kocha Mwinyi Zahera
Uongozi mpya chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla ulifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake ili kuepuka mgogoro huo ambao tayari ulikuwa umewasilishwa kwa mamlaka husika TFF
Hata hivyo Kakolanya amesisitiza kuwa yeye hakutaka kuondoka Yanga
Kakolanya amejitokeza kuwaomba radhi mashabiki wa timu hiyo wanaomtuhumu kuwa aligoma ili kuihujumu timu isifanye vizuri hasa ikizingatiwa alikuwa mlinda lango tegemeo
Kakolanya amekuwa akishushiwa tuhuma na baadhi ya mashabiki wa Yanga kuwa kwa kushirikiana na Wakala wake Suleiman Haroub ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, walitengeneza mgogoro huo ili kuinufaisha Simba
"Ni kweli kabisa hivi sasa mimi ni mchezaji huru na sina tena mkataba na Yanga kwani tayari umeshavunjwa na nishapewa barua inayoonyesha kuwa mimi ni mchezaji huru sasa," amesema
"Hata hivyo, nimekuwa nikipokea simu mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa Yanga wakinilaumu kuwa kuondoka kwangu ndiyo kumesababisha timu iwe hapo ilipo, ila naomba wajue kuwa siyo mimi niliyetaka niondoke"
"Lakini niwaombe tu msamaha kwa yote yaliyotokea kwani haya ni maisha tu, kwa hiyo haitapendeza kama kutakuwa na hali ya chuki dhidi yangu kutokana na hiki kilichotokea"
cut
Baada ya kuvunjwa mkataba wake, Kakolanya anatajwa kuelekea klabu ya Simba au Azam Fc dili hiyo ikisimamiwa na wakala wake Suleiman Haroub
Moja ya sababu iliyomfanya Zahera amuondoe Beno kikosini ni hii ya wakala wake kuwa kiongozi wa klabu ya Simba
Kwenye moja ya mahojiano yake Zahera alisema sio jambo zuri kwa Yanga kuwa na mchezaji ambaye msimamizi wake ni kiongozi wa Simba



0 Comments