Windows

David Bekham Apigwa Marufuku Kuendesha Gari

 

MWANASOKA maarufu wa zamani wa Uingereza, David Beckham,  amepigwa marufuku kuendesha gari kwa miezi sita baada ya kupatikana akitumia simu wakati akiendesha gari. Kapteni huyo wa zamani wa England amekiri makosa.

 

Mahakama imearifiwa kwamba alipigwa picha na raia mmoja akiwa ameshikilia simu wakati akiendesha gari lake aina ya Bentley ‘taratibu’ katika foleni.

 

Beckham, mwenye umri 44, ametozwa faini ya £750, ameagizwa alipe £100 gharama ya kesi na malipo ya ziada ya £75 katika siku saba zijazo.

 

Jaji katika mahakama hiyo amemwambia kuwa hata kama kasi ya gari ilikuwa taratibu kwenye foleni ‘hakuna kisingizio’ chini ya sheria.

 

Mwendesha mashtaka amesema: “Badala ya kutazama mbele na kuangalia barabara alionekana akitazama mapajani mwake.”

 

Wakili wa Beckham, Gerrard Tyrrell, amesema mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ” hakumbuki siku hiyo au tukio hilo”.

 

 

Aliongeza: “Hakuna utetezi wa kilichotokea, lakini mtazammo wake ni kwamba hakumbuki.” Tyrrell ameiambia mahakama kwamba Beckham hufurahia kuendesha gari.

 

“Huwapeleka watoto shuleni kila siku na mara nyingine hurudi kuwachukua anapoweza.”

 

Ni kinyume cha sheria nchini Uingereza kushika simu wakai unaendesha gari. Mtu anaweza kuadhibiwa kwa kupunguziwa pointi kwenye leseni na kutozwa faini ya £200 – lakini kutokana na uzito wa makosa anaweza kufikishwa mahakamani na akahukumiwa adhabu kali zaidi.

The post David Bekham Apigwa Marufuku Kuendesha Gari appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments