


KIUNGO wa Simba, Clatous Chama, amesema iwapo viongozi wa klabu hiyo watamwomba awatafutie wachezaji, atawaletea ‘visu’ hasa kutoka nchini kwao Zambia.
Akizungumza na BINGWA juzi, Chama alisema kuwa kuna wachezaji wengi mno wazuri na wenye uzoefu anaowafahamu ambao anaamini wakitua Simba, wataifanya timu hiyo kuwa tishio zaidi msimu ujao.
Hata hivyo, alikiri kikosi cha Simba kuwa na wachezaji wazuri mno, kuanzia wazawa na hata wa kigeni kiasi cha kuwawezesha kufanya vema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Katika kikosi cha Simba kuna wachezaji wazuri sana, ndiyo maana tumefanya vizuri msimu huu kimataifa na hata kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania.
“Lakini kama nikitakiwa kuleta wachezaji, wapo wengi ninawafahamu wenye uwezo wa juu ambao wakija wataisaidia sana Simba,” alisema kiungo huyo.
Chama alichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Simba kimataifa, akifunga mabao muhimu yaliyoiwezesha timu hiyo kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.



0 Comments