Windows

Djuma: Yanga ‘big up’


ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amewachambua Wanyarwanda waliosajiliwa na Yanga na kukiri Wanajangwani hao wamepata vifaa vya nguvu.

Wachezaji aliowazungumzia Djuma ni kiungo mshambuliaji, Issa Bigirimana kutoka APR na winga Patrick Sibomana, anayetokea Isonga FC zote za Rwanda.

Nyota hao wamemalizana na Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja, ikiwa ni mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, katika kuboresha kikosi hicho.

Akizungumza na BINGWA jana kwa mtandao kutoka Rwanda, Djuma, alisema anawafahamu vizuri wachezaji hao na kuwaambia Wanayanga wasubiri kuona mambo.

Djuma alimtaja Bigirimana kuwa mchezaji mwenye uwezo wa kufumania nyavu, zaidi ya alivyo straika wa Simba, Meddie Kagere, aliyemaliza Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 23.

“Kama Yanga imewasajili wachezaji hao, ni wazuri sana na wafahamu, Bigirimana amechezea APR ni kati ya wafungaji hatari Rwanda, tena kwa huko anaweza kumzidi hadi Kagere,” alisema Djuma.

Alisema klabu hiyo ya Jangwani imefanya chaguo sahihi kutokana na ushindani wa soka la Tanzania na kusema wachezaji hao wana uwezo mkubwa na damu zao ni changa, wote wakiwa na miaka 22.

Post a Comment

0 Comments