Windows

CAF yatangaza viingilio kutazama AFCON 2019




Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) inayotarajia kuanza mwezi ujao nchini Misri na Tanzania ikiwa ni miongoni mwa timu 24 zitakazoshiriki.

Gharama hizo zimewekwa katika madaraja mbalimbali ambapo kwenye michezo ya hatua ya makundi tiketi za daraja la kwanza zitakuwa ni USD 29 (TZS 66,000), tiketi za daraja la pili USD 18 (TZS 41,000) na tiketi za daraja la tatu USD 6 (TZS 14,000).

Katika hatua hiyo Taifa Stars itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria.

Kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja kwanza itakuwa USD 35 (TZS 80,000), daraja la pili USD 24 (TZS 55,000) na daraja la tatu USD 12 (TZS 28,000).

Hatua ya nusu fainali tiketi za daraja la kwanza zitakuwa ni USD 59 (TZS 136,000), daraja la pili USD 29 (TZS 66,000) na daraja la tatu USD 18 (TZS 41,000).




Mchezo wa mshindi wa tatu itakuwa ni USD 35 (TZS 80,000) daraja la kwanza, USD 24 (TZS 55,000) daraja la pili na USD 12 (TZS 28,000) daraja la tatu.

Katika mchezo wa fainali, tiketi za daraja la kwanza itakuwa ni USD 106 (TZS 244,000), daraja la pili ni USD 44 (TZS 101,000) na daraja la tatu USD 24 (TZS 55,000).

Taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na kutaja viingilio hivyo, imeeleza kuwa yeyote atakayehitaji kupata tiketi hizo awasiliane na shirikisho hilo mapema.

Post a Comment

0 Comments