Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amesema tangu awali alishasema kikosi hicho kitakuwa mabingwa na haitabadilika.
Aussems ametamka hayo baada ya kuibamiza Coastal Union ya Tanga mabao 8-1 na kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara, nafasi ambayo iliwang'oa Yanga kwenye kiti hicho.
Amesema, kipindi cha miezi ya Novemba na Desemba alisema juu ya hilo na ndivyo anasisitiza lakini hajajua lini.
"Kama nilivyosema awali ndivyo ilivyo, Simba itakuwa bingwa lakini sijui ni lini, tunachokifanya ni kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote zilizobaki,"alisema Aussems.
"Haijalishi kama tutapanda pointi zote sawa, pointi 20 au 15 lengo ni kuwa mabingwa tu."
Kwa sasa Simba imebakisha michezo saba ambayo kama watashinda yote watakuwa na pointi 21 pamoja na 81 walizonazo sasa zitakuwa 101.
Kama watashinda mitano watakuwa na pointi 15 na zitatosha kuwapa Simba ubingwa kwani Yanga waoshika nafasi ya pili na pointi 80 baada ya kucheza mechi 34 idadi sawa na matajiri wa Azam FC ambao wanashika nafasi ya tatu na pointi 67.
Yanga pamoja na Azam FC wote wamebakisha mechi nne ambazo ni sawa na pointi 12.

0 Comments