Windows

African Lyon washuka rasmi daraja





Klabu ya soka ya African Lyon ya jijini Dar Es Salaam leo imeshuka rasmi ligi kuu kwenda ligi daraja la kwanza mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Mbao Fc.


African Lyon wamepoteza mbele ya Mbao Fc wakicheza uwanja wa Uhuru kwa kufungwa bao 3 kwa 2 mabao ya washindi mbao yakifungwa na Mujwahuki, Pastory Athanas na Said Jr huku mabao ya African Lyon yakifungwa na Adil na Mtikila.

Kwa Matokeo hayo AFrican Lyon wamebakiza mechi 4 na hata wakishinda mechi zote watafikisha points 34 ambazo ni pungufu na timu iliyo kwenye nafasi ya pili kutoka Mwisho.

Post a Comment

0 Comments