Windows

YANGA YA MWINYI ZAHERA YAJIWEKEA REKODI YAKE FA KWA TIMU ZILIZOTINGA NUSU FAINALI


LICHA ya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali msimu huu na kuungana na timu nne zilizoshinda michezo yao ya kombe la Shrikisho, Yanga imetinga kwa hatua yao ya kibabe kwa timu zilizotinga hatua ya nusu fainali.

Timu zote nne ambazo zimetinga hatua ya nusu fainali kwenye michezo yao ya robo fainali zilipata ushindi ndani ya dakika 90 hali ambayo ni tofauti na Yanga ambao walilazimisha mpaka mwamuzi kuamua ipigwe mikwaju ya penalti.

Mpaka sasa timu ambazo zimetinga hatua ya nusu fainali ni pamoja na Lipuli FC, KMC, Azam FC na Yanga wenyewe  ambao ndio wenye uzoefu kwa sasa kwenye hatua hii ya michuano ya kombe la Shirikisho.

KMC ilishinda kwenye mchezo wake uliochezwa Uwanja wa Isamuhyo kwa mabao 2-0 dhidi ya African Lyon, Azam FC ilishinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba na Lipuli ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Singida United Uwanja wa Samora. 

Yanga ilishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Alliance baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kwenye nusu fainali Yanga itamenyana na Lipuli ya Iringa Uwanja wa Samora na Azam FC watamenyana na KMC uwanja wa Chamazi.

Post a Comment

0 Comments