Windows

BAADA YA KUNG'OLEWA NA YANGA FA, ALLIANCE WAHAMISHIA HASIRA ZAO HUKU


UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa kwa sasa hasira zao za kutolewa na Yanga hatua ya robo fainali kombe la Shirikisho wanazihamishia kwa Singida United kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa kesho uwanja wa Namfua.

Alliance walitolewa na Yanga hatua ya robo fainali kombe la shirikisho kwa kufungwa penalti 4-3 na Yanga mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba.

Ofisa Habari wa Alliance, Jacson Mwafulango amesema wanatambua ugumu wa kupata matokeo kwa sasa kwenye ligi ila hakuna haja ya kuwa kuwa na hofu wataaendeleza ubora wao kwenye ligi.

"Hakuna cha kuhofia kwa sasa kwenye ligi kuu, tunajua tumeshindwa kusonga mbele hatua ya nusu fainali FA ni mchezo tu na yale ni matokeo ila sasa tunahamishia nguvu zetu TPL kwa Singida United," amesema Mwafulango.

Alliance ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 30 imejikusanyia pointi 36 kibindoni.

Post a Comment

0 Comments