Windows

WAWILI WA KIMATAIFA WAZUA HOFU SIMBA


Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Jamhuri Stadium mjini Morogoro, kikosi cha Simba kimezidi kujifua kwa ajili ya mechi na JKT Tanzania.

Simba inacheza na JKT kesho Jumatano kabla ya kumenyamana na TP Mazembe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya jana yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Highland Bingwa mjini Morogoro, wachezaji Mzambia, Clatous Chama na Mganda Emmanuel Okwi hawakuwa sehemu ya mazoezi.

Chama na Okwi walikosekana na kuleta sintofahamu ya lini watawasili japo tarifa zimeelezwa kuwa tayari wameshajiunga na kikosi mjini humo majira ya jana jioni.

Kukosekana kwa Okwi na Chama katika mazoezi ya jana kumeleta hofu kama wanaweza kucheza mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania kutokana na kutoshiriki mazoezi kw asiku kadhaa.

Post a Comment

0 Comments