BAADA ya kupoteza mchezo wao wa hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho pamoja na ule wa kwanza wa ligi mbele ya Azam FC Uwanja wa Kaitaba, uongozi wa Kagera Sugar umepania kulipa kisasi kwa Azam leo.
Kagera Sugar msimu huu kwenye michezo miwili ambayo wamecheza na Azam hawajafanikiwa kupata matokeo hivyo wameamua kuhamishia hasira zao kwenye mchezo wa ligi.
Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Azam utakaochezwa uwanja wa Nyamagana.
"Tulipoteza mchezo wetu wa ligi wa awali na pia tukapoteza mchezo wetu wa kombe la Shirikisho ila kwa sasa hatuta kubali kupoteza tena mbele yao lazima tukaze.
"Hatupo kwenye nafasi nzuri ndani ya ligi hivyo ni lazima tupambane kupata matokeo, wachezaji nimewaambia na mapungufu kwa michezo yetu iliyopita tumeyafanyia kazi kilichobaki ni kupata matokeo chanya," amesema Maxime.
Kagera Sugar imecheza michezo 29 inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo baada ya kukusanya pointi 36.

0 Comments