NAHODHA wa timu ya Simba, John Bocco amesema kuwa bado wachezaji wataendelea kupambana kwenye mechi zilizobaki ili kupata matokeo chanya.
Jana Simba ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Biashara United, leo imerejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa uwanja wa Uhuru, Aprili 30.
"Wachezaji wote wanapambana kwa sasa kupata matokeo, ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo kama ambavyo nasi tunahitaji hivyo tutapambana zaidi kuendelea kushinda.
"Malengo yetu ni kuona tunafanikiwa kutetea ubingwa wetu ambao upo mikononi mwetu, uwezo tunao na inawezekana kwa kuwa tuna nia, kikubwa sapoti ya mashabiki," amesema Bocco.
0 Comments