Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda London Marathon kwa mara ya nne mfululizo huku Muingereza Mo Farah aliyetarajiwa kutoa ushindani mkali akimaliza katika nafasi ya tano.
Kipchoge, 34, ambaye alivunja rekodi ya dunia ya mbio za marathonn mjini Berlin mwaka jana, alikamilisha mbio za leo kwa muda wa saa mbili dakika mbili na sekunde thalathini na nane (2: 02: 38.)
Waethiopia Mosinet Geremew na Mule Wasihun walimaliza katika nafasi ya pili na ya tatu nyuma ya Kipchoge, ambaye alikosa kuvunja rekodi yake mwenyewe ya Dunia kwa sekunde 59 ambayo ilikua 2:01:39. Farah alimaliza mbio hizo dakika 3 na sekunde mojanyuma ya Kipchoge, huku Muingereza Callum Hawkins akimaliza katika nafasi ya 10.
Kwa upande wa wanawake, Mkenya Brigid Kosgei, 25, alishinda mbio hizo na kuwa mwanamke wa kwanza mwenye umri mdogo kushinda London Marathon upande wa wanawake. Mkenya mwingine Vivian Cheruiyot ambaye alishinda mbio za mwaka jana, alimaliza wa pili mbele ya Muethiopia Roza Dereje.
0 Comments