LEICESTER City leo wameichapa Arsenal mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa uwanja wa King Power na kuwapunguzia kasi ya kusaka nafasi ya kutinga nne bora.
Arsenal inapoteza mchezo wake wa tatu mfululizo leo kwa kufungwa idadi sawa ya mabao katika kila mechi ambapo walianza kufungwa na Craystal Palace wakiwa nyumbani mabao 3-2 Aprili 21 kisha wakapoteza mbele ya Wolves wakiwa nyumbani kwa kufungwa mabao 3-1 Aprili 24 na leo mbele ya Leicester City kwa kufungwa mabao 3-0 na kufanywa wafungwe jumla ya mabao 9 kwenye mechi tatu.
Mabao ya leo yaliyofungwa na Youri Tielemans dakika ya 59 na yale mawili yaliyopachikwa kimiani na Jamie Vardy dakika ya 86 na 90 yalitosha kuimaliza kabisa Arsenal nguvu.
Ushindi huu unaifanya Arsenal iwe nafasi ya tano baada ya kucheza michezo 36 ikibakiwa na pointi zake 66 huku Leicester City wakiwa nafasi ya nane baada ya kujikusanyia pointi 51 na wamecheza michezo 36.
Pia kwenye mchezo wa leo Arsenal walimalia wakiwa pungufu baada ya dakika ya 36 kwa Ainsley Maitland.

0 Comments