Windows

MANCHESTER CITY YAWASHA MOTO, YAISHUSHA LIVERPOOL KIBABE


MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa ushindi wa leo mbele ya Burnley haikuwa rahisi kutokana na ushindani mkubwa uliopo ndani ya Ligi Kuu ya England.
Manchester City wamerejea kwenye nafasi ya kwanza kwa kuishusha Liverpool ambayo ina ponti 91 baada ya kucheza michezo 36 huku wao wakiwa na pointi 92 baada ya kucheza michezo 36.
Bao pekee la ushindi leo limepatikana dakika ya 63 kupitia kwa Sergio Aguero aliyebutua mpira kwenda kwenye lango la mpinzani wake ambao licha ya mabeki kujitahidi kuokoa teknolojia ya goli ililikubali.
"Ilikuwa ni muhimu kwangu kushinda kutokana na namna tulivyocheza, tumemiliki vizuri mpira na hatujaruhusu hata kona moja, tumeruhusu mipira huru michache na kumiliki mpira hasa baada ya kipindi cha kwanza kwani mwanzo ilikuwa ngumu kwetu.
"Baada ya mapumziko tuliongeza nia ya kutaka kushinda kama tulivyofanya Old Trafford, ila kwa namna tulivyokuwa tunacheza nilijua tu lazima tutashinda, tulijua tunachokitaka na ndio maana tukawapa presha kubwa na kutengeneza nafasi nyingi, nafurahi kuona tumeshinda," amesema.


Post a Comment

0 Comments