Windows

AFC Leopards wawaparamia Bandari Machakos

Miamba AFC Leopards walivuna ushindi muhimu wa 2-1 dhidi ya timu ya Bandari katika mechi ya ligi kuu nchini Kenya -KPL siku ya Jumapili ugani Kenyatta mjini Machakos.

Vincent Oburu aliipa Leopards uongozi katika kipindi cha kwanza baada ya kuandaliwa pasi safi na Paul Were. Mshambulizi wa zamani wa Leopards Alex Orotomal aliisawazishia Bandari kabla ya Whyvonne Isuza kuipa Leopards ushindi kwa kufunga bao lake la saba mwezi huu wa Aprili.

Katika mechi iliyotangulia katika uga huo wa Machakos, Sofapaka na Mathare United zilitoka sare ya mabao mawili. Mganda Umaru Kasumba aliifungia Sofapaka mabao yote mawili naye Cliff Nyakeya akatia kimyani mabao ya Mathare United.

Mjini Kericho, Mt. Kenya United iliwachabanga Zoo 3-2. Hii ni licha ya wachezaji wa timu hiyo kuwa kwenye mgomo baridi kutokana na kutolipwa mishara yao.

Siku ya Jumamosi, Gor Mahia ilivuna ushindi wa 2-0 didhi ya Tusker. Nzoia Sugar iliilaza Chemelil Sugar 2-1 nayo KCB na Kakamega Homeboyz ikatoka sare ya moja moja. Sony Sugar iliichapa Western Stima 2-0 nayo Kariobangi Sharks na Postage Rangers walitoka sare ya moja kwa moja.

Mechi zaidi zitachezwa siku ya Jumatatu, Jumatano na Alhamisi.


Post a Comment

0 Comments