Windows

DABI YA WAJESHI ITANOGA KINOMA, HESABU ZA RUVU SHOOTING BALAA


UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kuona wanashinda kila mechi iliyo mbele yao kwani hali yao sio nzuri kutokana na nafasi ambayo wapo kwa sasa.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 33 imejikusanyia pointi 36 baada ya kushinda michezo 8 na sare 12 huku ikipoteza michezo 13.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Abdulmutik Haji amesema kuwa ushindani kwenye ligi ni mkubwa nao watapambana ili kupata matokeo.

"Sio kazi nyepesi hasa ukizingatia wote tuna asili moja hivyo kila mmoja atamkamia mwenzake ili kupata matokeo ila tupo tayari kupata matokeo.

"Nafasi ambayo tupo kwa sasa ni mbaya na ni lazima tupate matokeo chanya ili kujinasua hapa tulipo nina amini tutafanikiwa kufikia malengo yetu," amesema Abdulmutik.

Dabi ya wajenda hao kati ya RuvuShoting dhidi ya JKT Tanzania itapigwa Mei 3 mwaka huu uwanja wa Mabatini.


Post a Comment

0 Comments