Mashujaa FC ya mkoani Kigoma, itakumbukwa msimu huu kwa kuing'oa Simba yenye kikosi kipana kwenye michuano ya FA kwa ushindi wa mabao 3-2 uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Manyundo amesema kuwa walipambana kwa nguvu zote ili kupanda daraja msimu huu ila jitihada zao hazikuzaa matunda kutokana na kubanwa mbavu na timu pinzani.
"Unajua baaada ya kuwanyoosha Simba sasa wapinzani wetu wakajua kwamba sisi sio timu ya mchezo wakawa wanatukamia katika kila mchezo hali iliyofanya tushindwe kupeta kama tulivyoanza awali ila ninachoshukuru hatushuki daraja.
"Mchezo wetu wa jana dhidi ya Arusha tulishinda bao 1-0 hivyo tupo nafasi ya tano tukiwa na pointi 30 msimu ujao tutakuwepo kwenye ligi hivyo tuna muda wa kujipanga ili kupanda daraja," amesema Atungo.
0 Comments