Windows

SERENGETI BOYS WAPISHANA NA FUKO LA HELA TAIFA, CAMEROON WABEBA KOMBE

KIKOSI cha timu ya ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys kimepishana na fuko la hela leo kwa kushuhudia mshindi wa kombe hilo Cameroon akitwaa ubingwa wake kwenye ardhi ya Tanzania Uwanja wa Taifa.

Serengeti Boys ilitolewa kwenye michuano hii mapema kwenye hatua za awali baada ya kufungwa mechi zote tatu za kundi A na kumaliza ikiwa nafasi ya nne bila kuambulia pointi hata moja.

Michuano hiyo iliyoshirikisha timu nane leo imefika tamati uwanja wa Taifa na kushuhudia bingwa akiwa ni Cameroon aliyeibuka kidedea baada ya kushinda mbele ya Guinea.

Mchezo huo uliochezwa leo dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kumaliza bila kufungana na ndipo bingwa akapatikana kwa mikwaju ya penalti ambapo Camareoon walishinda penalti 5-3.

Timu nne ambazo zilitinga hatua ya nusu fainali ambazo ni Nigeria, Angola, Guinea na Cameroon zimevimba akaunti zao kwa kuingiza dola 75,000 (Tsh. 173,472,656), bingwa ambaye ni Cameroon amesepa na dola 150,000 (Tsh.346,954,144) na mshindi wa pili Angola ambaye alimshinda Nigeria jana kwa mabao 2-1 anavimba na dola 100,000 ( Tsh.231,302,752).

Post a Comment

0 Comments