Vinara wa Bundesliga Bayern Munich wametoka sare ya 1 – 1 nyumbani kwa Nurnberg na kuwapa Borussia Dortmund matumaini katika mbio za ubingwa, lakini mambo yangekuwa mabaya hata zaidi kama wenyeji wangefunga penalti waliyopoteza katika dakika ya mwisho.
Vijana hao wa kocha Nico Kovac ilijikuta nyuma katika derby hiyo ya Bavaria kupitia bao la Matheus Pereira.
Bayern walisawazisha wakati Serge Gnabry alifunga krosi ya Kingsley Coman. Lakini Tim Leibold alipoteza panalti katika dakika ya mwisho kwa kugonga mwamba wa lango.
Bayern ambao wanatafuta taji la saba mfululizo, sasa wako mbele ya Dortmund na pengo la pointi mbili, ambao walipoteza 4 – 2 dhidi ya Schalke huku zikisalia mechi tatu msimu kumalizika
0 Comments