Windows

Rais Magufuli aelezea namna anavyoumia timu za Tanzania zikifungwa


Rais John Magufuli ameelezea ushabiki wake wa soka akielezea namna anavyoumia pindi timu za Tanzania zinapofungwa na timu za ugenini. Rais Magufuli amemweleza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe namna anavyoumia timu za Tanzania zikifungwa, huku akisisitiza kuwa ni aibu wan chi yenye watu milioni 55 kufungwa na taifa lenye watu wachache.


Rais ameyasema hayo leo Aprili 30 mwaka 2019 katika viwanja vya Mwakangale wilayani Kyela ikiwa ni sehemu ya ziara yake inayoendelea sasa mkoani Mbeya.


“Waziri wa Michezo kwenye timu ya vijana ameniangusha, hili nasema kwa dhati yaani mpira uchezewe kwenye nchi yako, timu ya kwako halafu mnalishwa mabao mnatandikwa hapohapo mara mabao manne, mara mangapi yaania jabu kweli kweli nafuu ungechukua timu ya Kyela labda tusingefugwa hivi mabao.”


“Lakini katika vitu ambavyo huwa vinaniboa ni kufungwa kwa timu zangu, naumiaga mno… huwa najisikia hovyo. Kufungwa nyumbani ni aibu mkishafungwa wote milioni 55 na timu ina watu milioni 10 ni aibu, na waziri kwa kweli lazima utakuwa unaibeba hiyo aibu sijui mtaifuta lini kwani mkishafungwa mnaaibika wote,” amesema.


Amesema kwa kuwa kwa sasa timu ya Taifa inajiandaa na mchezo anatamani kuwa waziri wa michezo, “Sijui utaliwekaje sasa hivi tuna timu ya taifa inajiandaa sijui ikafungwe? Natamani siku moja niwe waziri wa michezo waone takavyokuwa timu nitaipanga mwenyewe.”

Post a Comment

0 Comments