Windows

Ishu ya jezi ya Taifa Stars yazua jambo, TFF yafunguka

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanza kupiga hesabu za haraka katika upatikanaji sahihi wa jezi halisi za timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ hapa nchini.
Taifa Stars imefanikiwa kufuzu katika Fainali za Afcon zitakazofanyika Misri, Juni mwaka huu, lakini kumekuwa hakuna jezi maalumu kwa mashabiki wake kiasi cha kuvaa jezi mbalimbali zenye nembo ya bendera ya Tanzania.
Katibu mkuu wa Shirikisho hilo, Wilfred Kidao aliliambia Mwanaspoti wameanza utaratibu wa kuhakikisha wananchi wanapata jezi mapema kabla ya kwenda katika Fainali za Afcon.
"Kila kitu kitakuwa wazi kesho, tutakuwa na mkutano hapa hapa lakini utaratibu huo upo na watu watapatikana katika mambo hayo ya jezi," alisema Kidao.
Aliongeza kwamba suala hilo haliwezi kulizungumzia kwa wakati huu kwani lipo chini ya kitengo cha fedha na bado wana vikao vinavyoendelea.
"Haya mambo yapo chini ya kitengo cha fedha, lakini kwa kifupi wameanza kufanyia kazi muda mrefu na kesho kila kitu kitakuwa wazi tutatangaza,'' alisema

Post a Comment

0 Comments