Windows

MASHINE NNE HATARI ZATAJWA KUTUA SIMBA KUCHUKUA NAFASI YA OKWI


Kufuatia uwepo wa tetesi kuwa Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Mganda, Emmanuel Okwi kutajwa kuwa anawindwa na Super Sport ya Afrika Kusini, imeelezwa mabosi wa klabu hiyo wapo kwenye mchakato wa kumpata mbadala wake.

Okwi ambaye ameichezea Simba kwa mafanikio alianza kuvutiwa rada na timu za Afrika Kusini mwaka jana ikiwemo Kaizer Chiefs lakini jitihada zao ziligonga mwamba kutokana na dau lake kuwa kubwa.

Taarifa hivi sasa zinasema tayari uongozi wa juu wa Simba umeshaanza mikakati ya kumsakala mbadala wake mwenye uwezo wa kuisaidia timu haswa katika michuano ya kimataifa.

Imetajwa kuwa mazungumzo baina ya klabu na Jacques Tuyisenge anayekipiga Gor Mahia yameanza huku pia straika Lazarous Kambole wa Zesco United naye akiwa kwenye mipango ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu braa.

Mbali na wawili hao, majina mengine yaliyotajwa ni Mzimbabwe Obrey Chirwa ambaye mkataba wake na Azam FC unamalizika mwishoni mwa msimu huu pamoja na Ibrahim Ajibu anayekipiga Yanga.



Post a Comment

0 Comments