Ofisa Habari wa zamani Yanga na sasa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, amewataka wanachama wa Yanga kuchagua viongozi makini ambao wataweza kuipa maendeleo Yanga.
Muro ameeleza kuwa kwa sasa Yanga imekuwa na makundi ambayo yamekuwa yanaiharibu klabu na ukiangalia ipo kwenye mashindano ya ligi na kombe la FA.
Muro amesema wanachama wanapaswa kuzingatia aina ya viongozi ambao wanaweza kuwa msaada mkubwa wa klabu ili kuisaidia kufika mbali kuliko kuiharibu.
Hata hivyo Muro amesema Yanga itakuwa inafanya uchaguzi katika kipindi kigumu kwakuwa itakuwa katikati ya mashindano ukiangali hivi sasa ipo kwenye ligi na FA.
"Ni vema Yanga wakaangalia kiongozi ambaye atajitoa kwa ajili ya timu na klabu kwa ujumla.
"Wanachama wanapaswa kuchagua kiongozi anayejitambua na atakayeleta maendeleo mazuri." amesema.
0 Comments