Windows

Mamelody Sundowns wapigwa na Wydad Casablanca

Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini imeanza kwa kipigo katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Wydad Casablanca ya Morocco kwa jumla ya goli 2-1.

Wydad walianza kwa kasi kubwa baada ya kufanya majaribio kadhaa golini mwa Mamelody licha ya Denis Onyango kuwa tatizo kubwa kwao. Onyango aliokoa mpira wa kichwa cha Salaheddine Saidi uliokuwa na madhara makubwa.

Pamoja na kasi ya Wydad, Mamelody walitengeneza nafasi chache kupitia kwa Gaston Sirino na Lebohang Maboe ingawa pia mlinda mlango wa Casablanca Ahmed Tagnaouti.

Baada ya kusubiri kwa mda, hatimaye kunako dakika ya 26 Wydad Casablanca ilipata goli la kuongoza kupitia goli la kushitukiza.

Kocha wa Mamelody Pitso Mosimane alikiongoza kikosi chake kupata goli la kusawazisha kwa kichwa kupitia kwa Ngcongca, goli lililomaliza kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili Wydad waliongeza kasi ya kushambulia iliyoisaidia kupata alama tatu na goli 2 ambalo sawa na moja.

Baada ya matokeo haya kwenye mchezo wa kwanza, mchezo wa mkondo wa pili Mamelody Sundowns watahitajika kushinda kuanzia goli mbili bila majibu.

Mchezo wa marejeano utafanyika wiki moja kutoka sasa. Tofauti na misimu mingine, msimu huu katika hatua hizi timu zote zimewai kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa katika nyakati tofauti.

Kikosi cha Mamelody Sundowns kilikuwa hivi:-

Sundowns: Onyango, Ngcongca, Lebusa, Nascimento, Langerman, Mabunda, Kekana, Morena, Zwane, Sirino, Maboe.

Akiba: Mweene, Arendse, Vilakazi, Lakay, Mahlambi, Coetzee, Soumahoro.

Jumamosi Aprili 27, 2019

Esperance De Tunis dhidi ya TP Mazembe, mtanange wa pili mkondo wa kwanza utaanzia Tunisia.


Post a Comment

0 Comments