Patrick Aussems, kocha wa Mkuu wa Simba amesema ushindi wa mabao 3-0 walioupata jana mbele ya Mbao sio mwisho wa mapambano kwa wachezaji wake kwani bado wana kazi ngumu ya kufanya kupata matokeo.
Mabao ya jana ya Simba yote matatu waliyapata kutokana na makosa ya mabeki wa Mbao, ambapo bao la kwanza lililopachikwa na John Bocco lilitokana na faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein na mabao mawili yalifungwa kwa penalti.
"Tulistahili kupata matokeo mbele ya Mbao jana, tulicheza vizuri,tulishambulia, tulimiliki mpira ndio maana tumepata matokeo ya ushindi,bado tuna kazi ngumu kwa wachezaji wangu kuendelea kupambana kwa ajili ya michezo inayofuata.
"Nina imani mashabiki na wa Simba watakuwa na furaha kutokana na matokeo yetu hilo ni jambo la kujivunia, wachezaji wangu wanastahili pongezi na bado tutaendelea kupambana," amesema
Jumatano Simba wataingia Uwanjani kumenyana na JKT Tanzania mchezo wa ligi kuu Bara, kwa sasa wamefkisha pointi 57 baada ya kucheza michezo 22

0 Comments