Windows

YANGA YATUMA UJUMBE MZITO KWA WAPINZANI WAO


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unatambua ushindani ni mkubwa ndani ya kombe la Shirikisho ila namna bora ya kuonyesha ukomavu wao ni kushinda kila mechi watakayocheza.

Yanga itaifuata Alliance kwenye mchezo wao wa hatua ya robo fainali Uwanja wa CCM Kirumba mchezo unaoatarajiwa kuchezwa wiki ya Machi 27 au 31.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema hakuna namna ya kuwazuia kwa sasa kutokana na kasi ambayo wapo nayo, licha ya kuwatambua vzuri Alliance wataonyesha utofauti.

"Linapofika suala la ushindani kila mmoja anatafuta matokeo, ila hesabu zetu hazijagoma na tutaleta ushindani kwa kila mchezo.

"Malengo yetu ni lazima yatimie, tunahitaji kufanya vizuri na kuleta ushindani katika kila mashindano ambayo tunashiriki kwa sasa, Alliance tunawaheshimu ila wanapaswa watambue Yanga ni timu kubwa," amesema Ten.


Post a Comment

0 Comments