Windows

AZAM FC: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA JKT TANZANIA


UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa kikosi kimejipanga leo kubeba pointi tatu mbele ya JKT Tanzania mchezo utakaochezwa Uwanja wa Chamazi leo.

Kocha wa Azam FC, Idd Cheche amesema anawaamini vijana wake watapata matokeo chanya kutokana na morali waliyonayo pmaoja na maandalizi waliyoyafanya.

"Tupo sawa hatuna tatizo kwa sasa, wachezaji wana morali kubwa na wanatambu kwamba tunahitaji ushindi hicho ndicho ambacho tutakifanya kwa wapinzani wetu.

"JKT Tanzania ni timu imara na yenye ushindani ila kinachodumu Uwanjani ni mbinu pamoja na kutafuata maotokeo hicho ndicho ambacho kitatubeba leo, tunahitaji pointi tatu," amesema Cheche.

Azam FC wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 53 kinara ni Yanga mwenye pointi 64.

Post a Comment

0 Comments