Windows

SERENGETI BOYS KUMALIZA UEFA ASSIST LEO DHIDI YA WENYEJI UTURUKI.....





Na Mwandishi Wetu, Uturuki
Kikosi cha Serengeti Boys, leo kimerejea uwanjani kuwavaa  wenyeji Uturuki.

Mechi hiyo inapigwa saa 5:30 asubuhi na muda mfupi ujao timu itatoka hotelini kwenda uwanjani.

Kikosi hicho kipo hapa mjini Antalya kushiriki michuano ya Uefa Assist yanayoendelea na tayari timu imecheza mechi mbili na kushinda moja na kupoteza moja.

Walianza kwa kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Guinea kabla ya kuamka katika mechi ya pili na kuwanyoosha Australia kwa mabao 3-2 katika mechi ya pili.


Katika mazoezi ya jana, Serengeti Boys walifanya yale mepesi lakini pia wakajifunza mbinu kadhaa katika umaliziaji pia ulinzi.

Post a Comment

0 Comments