NAHODHA wa timu ya Simba, John Bocco amesema hawana wasiwasi kuwavaa wapinzani wao JS Saoura kesho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya.
Simba kesho itacheza na JS Saoura nchini Algeria ikiwa ni mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
"Tumejiaandaa kufanya kazi kubwa kwa ajili ya timu yetu, maandalizi yetu ni mazuri na kila mmoja anatambua wajibu wake hivyo hatuna mashaka tunaimani tutafanya vizuri.
"Morali kwa wachezaji ni kubwa na mwalimu ametupa majukumu ambayo yatatusaidia kufanya vizuri, ni suala la wakati tu kupata matokeo," amesema Bocco.
Simba wapo kundi D ambalo kinara wake ni Al Ahly mwenye pointi saba, huku Simba akiwa na pointi sita nafasi ya pili na JS Saoura yupo nafasi ya tatu akiwa na pointi tano, AS Vital ana pointi nne nafasi ya nne.
0 Comments