Windows

MIPANGO YA STARS KUIMENYA UGANDA NI MOTO


IKIWA zimebaki siku 13 kabla ya timu ya Tanzania ya Taifa 'Taifa Stars' kumenyana na Uganda kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Afcon, kocha wa Stars, Emmanuel Amunike ameibuka na kubainisha mipango yake.

Mpaka sasa tayari wapinzani wa Stars, Uganda wameshatangaza kikosi chao cha awali ambacho kitamenyana na Stars Machi 22, Uwanja wa Taifa, huku Amunike akitarajiwa kutangaza  kikosi chake leo.

Amunnike amesema kuwa utaratibu wa kujiandaa kuelekea mchezo huo unaendelea, hivyo taratibu zikikamilika kila kitu kitakuwa wazi.

"Kwa sasa tunafanya kazi ya maandalizi ya Afcon kwa mipango tukiwa na hesabu za kusonga mbele tupo imara na tuna mipangi imara," amesema Ammunike.

Stars ipo kundi L ikiwa na pointi tano sawa na Lesotho ambao wapo nafasi ya pili huku vinara ni Uganda wenye 13, Cape Verde wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi nne.

Post a Comment

0 Comments