KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kuwa na kasi ya ajabu kwenye ufungaji ni watu ambao wamemzunguka akiwa Uwanjani.
Zahera amesema kuwa mshambuliaji yoyote anayefunga mabao mengi kwa wakati mmoja anaandaliwa na wachezaji walio nyuma yake pamoja na juhudi binafsi.
"Kwa sasa unaona tayari Kagere wa Simba yupo sawa na Heritier Makambo wa Yanga, haina tofauti kubwa sana zaidi ni watu wanaomzunguka ndio wanaomfanya awe hivyo.
"Kama anapata mipira kutoka kulia na kushoto sasa kwa nini asifunge? hapo ujue ana watu kama Chama (Claytous) Bocco (John) basi ni lazima afunge tu hamna namna," amesema Zahera.
Kagere ana mabao 12 kwenye ligi sawa na Makambo huku kinara akiwa ni Sallim Aiyee wa Mwadui FC mwenye mabao 14.
0 Comments