Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Dar es Salaam kikitokea Mwaza ambako kilicheza mchezo wa robo fainali wa kombe la Azam Sports Federation Cup na kushinda kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.
Baada ya kurejea Kocha mkuu Mwinyi Zahera amewapa mapumziko wachezaji wake kwa leo na kesho asubuhi wataendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi kurasini.
Mazoezi hayi yataanza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC April 04 katika dimba la Nagwanda Sijaona Mtwara.
Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho jana na sasa itacheza dhidi ya Lipuli Fc kwenye mchezo ujao utakaopigwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.
0 Comments