SAID Junior, mshambuliaji wa Mbao FC ambaye alifanikiwa kuipa ushindi timu yake walipocheza na Simba mzunguko wa kwanza amepania kufanya makubwa leo Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Junior amesema wamejipanga kiasi cha kutosha na wapo tayari kuonyesha ushindani kutokana na umuhimu wa mchezo na hesabu zao ni kuona wanashinda.
"Tupo vizuri na tumejipanga sawasawa hatuna hofu yoyote, nakumbuka mzunguko wa kwanza nilipata bahati ya kuifungia timu yangu, hivyo itakuwa vema pia nikipata nafasi leo na kuitumia kwa ajili ya ushindi wa timu yangu.
"Mchezo utakuwa mgumu ila kikubwa ni dakika 90 ndio zitaamua, mashabiki wajitokeze kwa wingi tunatambua ni timu ya aina gani ambayo tunakutana nayo sisi tupo tayari," amesema Junior.
Junior amepachika mabao 7 mpaka sasa TPL na ni kinara kwa upande wa Mbao FC kwa sasa.
0 Comments