

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa wanachosobiri hivi sasa ni dakika90 pekee za kuonesha kuwa wapo kwenye ligi kwa ajili ya kupigania ubingwa.
Yanga inashuka dimbani leo kucheza dhidi ya Alliance FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kuelekea mchezo huo, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema wameshakamilisha maandalizi yao na kinachosubiriwa hivi sasa ni mchezo wenyewe.
Amesema Alliance wanaichukulia kama timu zingine zinazoshiriki ligi na akieleza hivi karibuni wameanza kuja vizuri hivyo hawatakuwa na budi kupambana zaidi.
"Tunaenda kucheza na Alliance ambayo ni timu nzuri, imeanza kuja vema hivi karibuni japo tunaichukulia kama timu zingine.
"Tutajitahidi kupambana kadri ya uwezo wetu ili kujiwekea nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwani tumekuja hapa Mwanza kusaka alama 3" alisema.




0 Comments