Windows

Wasituzoee;Yanga watamba kuikalisha Alliance mapema.

ITAJUTA klabu ya Alliance ndivyo naweza kusema baada  ya Uongozi wa  Yanga kumesema  umejipanga vizuri kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Alliance wa kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba huku wakitamba kuinyamazisha timu hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa wanaiheshimu Alliance ila hawaoni tatizo litakalowaogopesha kushindwa kupata matokeo.

“Unapozungumzia Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wenye uzoefu, linapokuja suala la kutafuta matokeo ni lazima tupambane.

“Ni kikosi kizuri tumecheza nao na tunawatambua ila watatusamehe, tumejipanga kupata matokeo, nina imani ushindani utakuwa mkubwa, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna itakavyokuwa,” amesema Ten.

Yanga ikipenya itatinga nusu fainali na kukutana na Lipuli ya Matola ambayo tayari imekata tiketi kwa Singida United, Alliance nao watalazimika kwenda Samora kumenyana na WanaPaluhengo hao endapo watashinda kesho.


Post a Comment

0 Comments