Windows

Wakenya tayari kupambana katika mbio za nyika Denmark

Mashindano ya dunia ya mbio za nyika yatakayofanyika nchini Denmark yataanza hapo kesho Jumamosi saa saba mchana kwa saa za Afrika Mashiriki huku Wakenya wakilenga kutetea ubingwa wao walioutwaa mwishoni mwa mwaka wa 2017 huko Kampla Uganda.

Hata hivyo timu za wachezaji chipukizi hazijawa na ufanisi mkubwa huku mara ya mwisho ikiwa mwaka 2013 ambapo Faith Chepng‘etich aliipa Kenya dhahabu kwenye mbio za kilomita 6 kwa chipukizi ila kwa sasa chipukizi hao wanamini watakuwa na matokeo ya kupigiwa mfano.

Maneno sawa na hayo yamesemwa na meneja wa timu hiyo Benjamin Njoga anayeamini kuwa vijana wa sasa wana uwezo mkubwa wa kufanya vyema kuliko mwaka wa 2017

Aidha, kocha mkuu wa timu hiyo David Letting anasema timu yake ipo tayari kuletea Kenya fahari kwa kuUtetea ubingwa wao. Huko Uganda, Kenya ilizoa jumla ya medali 12.


Post a Comment

0 Comments