Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Daktari wa wachezaji, Yassin Gembe, umetangaza kuwa maendeleo ya wachezaji wake, Emmanul Okwi na Erasto Nyoni kuendelea vizuri.
Gembe amesema wachezaji hao hawakusafiri na timu kuelekea Algeria kwa ajili ya mechi na JS Saoura ambayo ilimalizika kwa Simba kufungwa mabao 2-0.
Gembe amesema wawili hao watakuwa Bocco Veterani leo kwa ajili ya mazoezi na ikiwezekana wakawa sehemu ya mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita.
"Nyoni na Okwi watakuwa wanafanya mazoezi leo kwakuwa hali zao zinaendelea vema na wanaweza kuwa sehemu ya kikosi dhidi ya Vita kama Mwalimu akiwapendekeza."
Simba itaenda kucheza na Vita Jumamosi ya wiki hii kusaka tiketi ya kufuzu kuelekea hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
0 Comments