Windows

VIDEO: WANAOKWAMISHA UCHAGUZI YANGA WATAJWA


Wanachama wa klabu ya wameazimia kwa pamoja kuchukua hatua za kisheria kwa watu wanaojaribu kukwamisha harakaati za uchaguzi wa klabu hiyo ambao mpaka sasa haujafanyika kwa sababu za mvutano na shirikisho la soka nchini TFF

Mratibu wa Matawi ya Yanga mkoa wa Dar es salaam Kaisi Edwin amesema viongozi wa juu wa tasisi zinazosimamia michezo nchini wameshindwa kutatua suala hilo kutokana na kutanguliza masirahi binafsi badala ya kutenda haki.


Katika hatua nyingine Edwin amelishushia lawama shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kile alichodai ni kuididimiza klabu hiyo baada ya kupigwa faini ya Jumla ya Tsh: million 8 kwa kukiuka kanuni za ligi kuu Tanzania bara.

Yanga imekua katika changamoto kubwa ya kiuchumi na kiuomgozi kwa muda mrefu sasa tangu kujihuzuru kwa aliyekua mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji katikati ya mwaka juzi, kutokana kukumbwa na changamoto za kiafya.


Post a Comment

0 Comments