Leo Yanga watakuwa mzigoni kumenyana na Alliance FC mchezo wa hatua ya robo fainali kombe la Shirikisho Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na watakosa huduma ya wachezaji sita wa kikosi cha kwanza.
Kwa mujibu wa kocha mkuu, Mwinyi Zahera amesema kuwa hana hofu na mchezo licha ya kukosekana kwa nyota wake wa kikosi cha kwanza.
"Juma Abdul, Mohamed Banka, Haji Mwinyi, Ibrahim Ajibu hawa wamebaki Dar, Gadiel Michael yeye amekwenda Afrika kusini kwa ajili ya majaribio, Ramadhan Kabwili yupo timu ya Taifa chini ya miaka 20.
"Sina mashaka nipo tayari kwa mchezo wangu wa kesho na nimewaambia wachezaji wangu wapambane na tutapata matokeo kila kitu kinawezekana," amesema Zahera.
0 Comments