MAANDALIZI ya michuano ya Afcon mwaka 2019 kwa vijana chini ya miaka 17 (U 17) itakayofanyika mwezi ujao yamezidi kupamba moto ambapo Uwanja wa Uhuru umewekwa kapeti jipya.
Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa ambayo inatambulika na Shirikisho la Mpira Afrika (Caf) hali ambayo inaongeza thamani ya mpira wa Tanzania kukua kwa sasa.
Kazi iliyopo kwa sasa ni kumaliza kupaka gundi maalumu iliyo chini ya wachina wanaokwenda kwa kasi ya hali ya juu na umakini.
Meneja wa Uwanja wa Uhuru, Nsajigwa Gordon amesema kuwa maandalizi yanakwenda sawa na ni ndani ya siku chache kila kitu kitakamilika.
"Maandalizi yanazidi kupamba moto kwa sasa tumefikia hatua nzuri na mafundi wanaendelea na kazi ya kutandika kapeti, baada ya siku nne kazi itakuwa imekamilika ya kutandika kapeti," amesema Gordon.

0 Comments