Uongozi wa klabu ya Singida United umepingana na kauliza Makocha wao baada ya kueleza kuwa wanashindia ndizi mbivu na wamekuwa hawapewi fedha za nauli kuelekea mazoezini.
Siku mbili zilizopita Kocha Mkuu wa timu hiyo, Msebria Goran Popadic, alisema wamekuwa hawatimiziwi mahitaji yao muhimu ikiwemo nauli na mlo huku akieleza wamekuwa wakila mpaka ndizi kutuliza njaa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida United, Festos Sanga, ameibuka na kukanusha malalamiko ya Makocha hao kuwa si ya kweli.
Sanga ameeleza kukiri kuwa ni kweli Singida inakabiliwa na ukata wa fedha lakini haijafikia hatua ya kushindwa kuwapa Makocha wake fedha za nauli na vyakula.
"Ni kweli timu ina ukata lakini si kweli yale yaliyozungumzwa na Makocha, hatuwezi kuwafanyia hivyo, wanapata mahitaji yote muhimu." alisema Sanga.
0 Comments