PASCAL Wawa, beki wa Simba amesema kuwa wapo tayari kupambana na timu yoyote kwa sasa kwenye ligi ili kupata matokeo na hilo linawezekana kutokana na sapoti ya mashabiki.
Simba kesho watakuwa kibaruani kumenyana na Mbao FC, uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Mbao Uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Wawa amesema kuwa anatambua kwamba ushindani kwenye ligi ni vita kubwa na kila timu inapambana kupata matokeo hivyo nao wanaingia vitani kupata matokeo.
"Tuna mechi nyingi kubwa na ngumu halafu zote za muhimu, sasa ili kuwa katika nafasi nzuri ni lazima tupate matokeo na hilo ndilo lengo letu.
"Nataka kuona mashabiki wakiwa na furaha, kila baada ya kumaliza mazoezi huwa natumia muda mwingine kufanya mazoezi magumu kujiimarisha zaidi, hivyo wapinzani wetu wajipange," amesema Wawa.
0 Comments